Wananchi zaidi ya 5000 wamefunga mwaka 2022 kwa kuagana na shida ya maji katika vijiji vya Ngámbi na Mbugani katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Hiyo ni kutokana na kujengewa visima virefu vya maji kupitia mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBBAR), mradi unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais .
Visima hivyo vimezinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selelmani Jafo hivi karibuni.
Bi. Elena Mpanda mkazi wa kijiji cha Mbugani amesema kuwa sasa shida ya kufuata maji wilaya ya jirani ya Kongwa na kuyanunua kwa shilingi 1,500/= kwa dumu imekuwa historia!