Mbunge wa Kigamboni, Dr. Faustine Ndugulile ameiomba serikali kuondoa tozo kwa vyombo vya moto vinavyovuka Daraja la Nyerere Kigamboni na mzigo huo wa deni la NSSF ubebwe na serikali.
“Wananchi wa Kigamboni hawana mbadala wa njia, ili mwananchi wa Kigamboni ili afike mjini analipa tozo, daladala moja inayopita pale inalipa 5,000, wananchi wa Kigamboni ili wafike mjini wanahitaji ruti tatu hadi nne, wananchi wa Kigamboni wamesikia kwamba daraja la Tanzanite litakuwa bure, wakazi wa Kigamboni ambao ni maskini wanatozwa tozo ili wavuke kwenda mjini na hawana mbadala kama wakazi wa Oystrebay na Masaki,sisi ukipita kwenye kivuko na darajani lazima ulipie, wananchi wamenituma kwa nini ni wao pekee yao wanatakiwa kulipia?” Ndugulile