Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amesema serikali ipo mbioni kukamilisha mkakati wa biashara mtandaoni ambao utawezesha wafanya biashara nchini kuuza bidhaa zao.
Akifunga maonyesho ya wiki ya viwanda katika viwanja vya Bunge, amesema biashara ni imani, uadilifu na kuwasihi wafanyabiashara nchini kuwa waaminifu wanapouza bidhaa kupitia mtandao.
Aidha, amesema anatamani kuona mchango wa sekta ya viwanda unachangia kwenye uchumi wa viwanda kwa asilimia 20 kwa mujibu wa sera ya viwanda badala ya asilimia moja iliyopo sasa.
Naye, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono ya kuhakikisha sekta binafsi inakuwa sehemu ya kuchangia uchumi wa nchi.