“Kuhusu chanjo dhidi ya corona Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake kuendelea na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru dhidi ya corona kwa kutumia chanjo zilizooridhiwa na (WHO) ili kuwapa fursa ya kinga Wananchi wake kwani kupitia uchambuzi wa Kamati chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi” Mwenyekiti wa Kamati Profesa Said Aboud
“Kipumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya corona nchini kwa kuanzia liwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu. Wahudumu wa Afya na Watumishi waliokatika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma, Watumishi wa Sekta ya Utalii, Hoteli, mipakani, Viongozi wa Dini na mahujaji” Mwenyekiti wa Kamati Profesa Said Aboud
“Wazee watu wazima kuanzia umri wa miaka 50, watu wazima wenye maradhi sugu ikiwamo sukari, matatizo ya upumuaji na wasafiri wanaokwenda nje ya nchi” Mwenyekiti wa Kamati Profesa Said Aboud
“Kufanya uhamasishaji wa maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na Wananchi wawe huru kuamua kuchanjwa au la,” Mwenyekiti wa Kamati Profesa Said Aboud