Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaajiri walimu wapya wa masomo ya sayansi na itaendelea kuboresha maslahi yao.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Skuli ya ghorofa ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh iliopo Monduli, Wilaya ya Magharibi A , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2024 ikiwa ni shamrashamra za Miaka ya 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amewapongeza Wizara ya Elimu kwa kazi nzuri ya kuvuka malengo ya ilani ya utekelezaji ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa ujenzi wa miundombinu ya Skuli ina lengo la kuboresha ili kupunguza msongamano wa wanafunzi na kutozidi idadi ya 45 kila darasa.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewataka wananchi kuendelea kuudumisha Muungano ili kupata maendeleo katika nyanja zote.