Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri sekta ya mitaji ili kuendeleza kuwezesha Watanzania na kuweza kuinua pato la Taifa.
Hayo ameyabainisha leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mfuko wa pamoja wa Timiza Unit Fund unaotoa fursa kwa Watanzania wenye kipato cha chini kuwekeza katika masoko ya mitaji na dhamana.
Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana imethibitisha kushusha kiwango cha chini cha ushiriki katika uwekezaji kwenye mfumo wa timiza kutoka Tsh. Million 1 hadi Elfu 10 lengo kuongeza ushiriki wa wekezaji wa kanda mbalimbali hasa kwa wawekezaji wa chini.
Timiza Fund ni mfuko wa uwezeshaji unaoendeshwa na Taasisi za ZENSECURITY pamoja na MWANGA BANK