Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini, sambamba na kuifungua nchi, ili wafanyabiashara waendelee kunufaika na fursa zilizopo kwa kufanya Biashara zao kwa uhuru ndani na nje ya nchi.
Profesa Mkumbo ameyasema hayo katika hafla ya utoaji Tuzo za Viwanda na Biashara kwa wanawake wajasiriamali.
Aidha amewahimiza wanawake kuendelea kuungana katika vyama vyao ili kuzifikia kwa haraka fursa za uchumi, kwani wanawake wengi wana uwezo wa kufanya Biashara na kupambana na viatarishi mbalimbali.