Wizara ya katiba na sheria imesema utekelezaji wa mpango mkakati wa utoaji elimu ya katiba utasaidia kuongeza uelewa wa wananchi juu ya katiba ambao kwa sasa ni asilimia 50 huku ikitangaza kuendeleza mchakato wa katiba uliokwama mwaka 2014
Akizungunza leo jijini Dar es salaam, katika mkutano na wadau wa sheria ikiwemo mawaziri wastaafu, Waziri wa katiba na sheria dokta Damas Ndumbaro, amesema katika utekelezaji wa mkakati huo wa elimu ya katiba, watawafikia watanzania kila maeneo, akisema mchakato wa katiba mpya utaendelea ulipoishia mwaka 2014 huku akisistiza upatikanaji wa katiba utazingatia mahitaji ya haki za binadamu na si shinikizo la watu
Kwa upande wake waziri katiba na sheria kutoka serikali ya mainduzi ya Zanziba Haroun Sueleimani amesema ushiriki wao katika mkutano huo ni kupata maoni juu ya mapendekezo katika baadhi ya maeneo ya katiba ya sasa kutokana na katiba hii kuhitaji marekebisho ya baadhi ya vipengele na si katiba yote
Naye mmoja wa mawaziri wastaafu aliyeshiriki katika mkutano huo Dokt Merry Nagu amesema maamuzi ya upatikanaji wa katiba mpya yanapaswa kuangalia matakwa ya sasa ikiwemo mahitaji ya jamii ya watanzania