Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea na taratibu za uwekezaji kwa kuongeza vituo vingine 4 kwa kujenga majengo na kuviwezesha vifaa vitakavyotumika kutibu wagonjwa wa Saratani kwa njia ya mionzi.
Waziri Ummy Mwalimu amesema hayo leo Aprili 5,2024 kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha Nne wakati akijibu swali namba 6,133 kutoka kwa Mbunge wa Vito Maalum Mhe. Tunza Issa Malapo aliyeuliza ‘Je ni Hospitali ngapi zinatoa huduma ya tiba ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani hapa nchini.
Amesema, kwa sasa Serikali ina jumla ya vituo Vinne ambavyo vinatoa huduma ya matibabu ya Saratani nchini kwa njia ya Mionzi, vituo hivyo ni Taasisi ya Saratani Ocean Road, Hospitali ya Kanda Bugando, Hospitali ya binafsi Besta na Hospitali ya Good Sammaritan (St. Fransis Ifakara).
“Serikali inaendelea na taratibu za uwekezaji kwa kuongeza vituo vingine 4 kwa Tanzania Bara katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, KCMC, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Hospitali binafsi ya Agakhan) na kimoja kwa Visiwani Zanzibar (Hospitali ya Binguni) kwa kujenga majengo na kuviwezesha vifaa vitakavyotumika kutibu wagonjwa wa Saratani kwa njia ya mionzi.” Amesema Waziri Ummy