Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ameishauri Serikali kusimamia mifumo inayounganisha sekta ya maliasili na utalii ili isomane hatua itakayosaidia kuongeza mapato kwa serikali pamoja na kupunguza migogoro baina askari wanyama pori na wafugaji nchini.
Cherehani ameyasema hayo Novemba 8, 2023 Bungeni Jijini Dodoma na kuongeza kuwa Serikali inapoteza fedha nyingi kwa kulinda na kutunza maeneo yasiyokuwa na vivutio wala wanyama bila kunufaika na mapoto yeyote huku madhara yake yakiwa ni kugombana na wananchi sambamba na kutengeneza matabaka baina ya askari wanyama pori na wananchi.
“Migogoro inazidi kuongezeka kwasababu Wafugaji hawana maji wala maeneo ya kuchungia mifugo yao hivyo ziwepo gharama za kuchunga kwenye maeneo yasiyokuwa na vivutio wala wanyama jambo ambalo litaongeza mapoto na kupunguza migogoro baina ya askari wanyama pori na Wananchi”.