Serikali mkoani Pwani, imeagiza wawekezaji wanaohitaji kuwekeza Mkoani humo waende kuhodhi maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji pamoja na kongani ,ili kuepuka kufanyiwa utapeli na kununua maeneo yaliyo kwenye migogoro ya ardhi.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge wakati alipokagua na kutembelea ujenzi wa mradi wa Kiwanda Cha Kinglion Steel kinachojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa zitokokanazo na chuma,huko Zegereni,Kibaha.
“Uwekezaji mkubwa kama huu unahitaji miundombinu yenye gharama,mfano barabara,maji,umeme wa kutosha,gesi ya kutosha, Kwahiyo tuna waambia wawekezaji wetu,vitu hivi ni gharama kubwa”
Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi huo, Arnold Christian Lyimo , meneja Kinglion Investment co.ltd anasema kukamilika kwa Kiwanda hicho kitakuwa ni kikubwa Afrika Mashariki na Kati.
Alieleza, ujenzi ulianza march 2022 na utakamilika April 2024 na kitaanza uzalishaji Juni 2024 na kitagharimu Bilioni 163.