Serikali iko mbioni kuanza kujadili kuweka kumbukumbu ya picha Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan kwenye fedha ya Tanzania ikiwa ni heshima ya kuwa na Rais wa kwanza mwanamke na kutambua utendaji wake.
Hayo yamesemwa Bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa @kassim_m_majaliwa wakati akijibu swali wa Viti Maalum Vijana Ng’wasi Kamani @ngwasi_kamani aliyetaka kujua ni lini serikali itaweka kumbukumbu ya kudumu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka picha yake kwenye fedha za nchi na kutambua mchango wa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania
“Maamuzi ya kuweka picha kwenye noti mara nyingi yanafanywa na maamuzi ya kiongozi mwenyewe kwakushauriana na benki kuu na sisi tunatambua kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mchango mkubwa katika Taifa hili na litaingia serikalini na litajadiliwa pale ambapo litafanyiwa maamuzi kwa kushirikiana na benki kuu taarifa zitatolewa rasmi” Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa JMT