Ikiwa imepita zaidi wiki kadhaa tangu wananchi waishio wiliya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kukumbwa na mafuriko ya maji hali iliyopelekea kupoteza makazi yao na mazao huku watu nane wakipoteza maisha,Serikali wilayani humo imeanza kugawa viwanja vya makazi 600 vilivyopimwa burevilivyopo kijiji cha Muhoro kwa wananchi ambao wapo tayari kuhama katika maeneo yao ya zamani yaliyozungukwa na maji.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ambapo amesema mpaka sasa wanaendelea na zoezi la ugawaji bure wa maeneo hayo mia sita na baadhi wameshapewa huku wakiendelea kupima viwanja vingine 500 vilivyopo kijiji cha Chumbi ili kugawia wananchi wengine ambao wapo tayari kutoka katika sehemu hatarishi yanayokumbwa na mafuriko.
Meja Gowele ameongeza kua mpaka sasa ni zaidi ya kaya 23000 ambazo makazi yao yamekubwa na mafuriko hayo ambapo kwasasa wengine wanaishi katika makambi maalumu yaliyoandaliwa sehemu mbili tofauti.
Mkuu wa Wilaya amesema hayo wakati akipokea misaada mbalimbali ya chakula,magodoro,vinywaji,vifaa vya tiba na mbegu kutoka kwa watu wa Who is Hussein waliogusa na wahathirika hao na kuwaomba wanajamii wengine wenye uwezo kuendelea kusaidia vitu mbalimbali kama chakula,magodoro na mahitajiengine ili viweze kusaidia jamii hiyo kwani kwasasa wanauhaba wa mafuta ya kuendeshea magari ambayo yanasaidia kupeleka vyakula kwa wahathirika ambao wapo mbali na mji wa ikwilili kwa kata za mbali zaidi.