Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan imepongezwa na Kufuruahishwa na Mkakati wa ulejeshwaji Mtoto wa kike Kuendelea kubaki shuleni hasa wale waliopitia changamoto mbalimbali na kusema imesaidia watoto hao kupata haki zao za kuendelea na Masomo.
Akizungumza Mara Baada ya kukamilika kwa Mashindano mbalimbali ya kimichezo yaliyoshirikisha Mtoto wa kike katika kuzingatia haki yake yaliyoandaliwa na shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na Shirika la Plan International kwa ufadhiri wa serikali ya Canada wameendelea kumwezesha mtoto wa kike ambapo Meneja Mradi wa shirika la Rafiki SDO ,Eliud Mtalemwa ameshukuru mwitikio uliofanywa na Serikali katika kuona mtoto wa kike anastaili kupata elimu.
Mashindano hayo ya Mpira yamefanyika wilayani Geita katika kata ya kasamwa ambao timu mbalimbali za wanaume zimeshiriki pamoja na Fainali ya mashindano hayo kama chachu ya kuleta hamsa kwa mtoto wa kike na kuona na yeye ana haki ya kupata elimu kama wengine.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya kasamwa Halmashauri ya Mji wa Geita Bi, Suzana Mjigaga amesema hadi sasa shule ya kasamwa imefanikiwa kuandaa chumba kwa ajili ya wanafunzi waliokuwa wamekatisha masomo na hii ni Baada ya matokeo ya Mradi huo Hata hivyo baadhi ya wananchi pamoja na wanafunzi wameeleza manufaa ya mradi kwa watoto wa kike