Serikali ya Burundi na Umoja wa Mataifa wametoa wito wa msaada wa kifedha ili kukabiliana na athari mbaya ya mvua mkubwa inayonyesha na ambayo imesababisha karibu watu 100,000 kuyahama makazi yao katika nchi hiyo.
Burundi ni miongoni mwa nchi 20 zilizo katika hatari kubwa ya kukabiliwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, imekumbwa na mvua isiyo na kikomo tangu mwezi Septemba mwaka jana, huku mji wake mkuu wa Bujumbura ukiharibiwa pakubwa na mafuriko kutokana na ujazo wa ziwa Tanganyika kuongezeka.
Eneo la Afrika Mashariki limekuwa likikumbwa na mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni ambazo zimegharimu maisha ya takriban watu 58 nchini Tanzania tangu kuanza kwa mwezi huu huku wengine 13 wakifariki nchini Kenya.