Serikali ya DRC imetangaza hatua ya kuorodhesha makanisa kwenye eneo nzima la Jimbo la Kivu ya kaskazini na kufunga yale ambayo hayajafuata masharti kisheria kwa lengo la kiusalama.
Mbele ya waandishi wa habari huko Goma, Naibu Waziri Mkuu anayesimamia mambo ya ndani Peter Kazadi alibaki imara kutangaza hatua hiyo
Hatua nyingine ni utambulisho wa makanisa yote yanayofanya kazi katika jimbo lote la Kivu Kaskazini. Baada ya kutambulishwa, tutawafunga yale makanisa yote ambayo hayatumiki kulingana na sheria.
Hatua hiyo inahusu makanisa na madhehebu yote ya Kivu Kaskazini ingawa ni vigumu kwa sasa kusema idadi yao haswa.
Mkuu wa parokia ya kimataifa ya kiinjilisti ya Goma Mchungaji Marcel Muhongera anaunga mkono mtazamo wa serikali
‘Sikubaliani kamwe na kufungwa kwa makanisa ya dini yoyote lakini siku zote nimekuwa nikihimiza kila mtu anayeanzisha dini kuwa na umoja na serikali’.
‘Nchi yetu ni ya kidunia lakini ikitokea mchafuko wa umma, serikali nayo ina haki ya kuitazama dini hii huko. Uhuru ni tofauti na uasherati’
Kiongozi wa makanisa ya uamsho katika jimbo la Kivu Kaskazini, askofu mkuu Josué Amurani, aliongoza ujumbe wa madhehebu ya kidini ambao ulikutana na ujumbe wa serikali Jumanne ambapo ameonya kutumia tahadhari wakati wa kuorodhesha makanisa
‘Tuko katika kipindi kigumu, nyeti sana ambapo tunahitaji tahadhari nyingi, hekima nyingi, kujizuia sana ambapo hatupaswi kutumia nguvu nyingi kufikia malengo’.
‘Ni lazima serikali iwe na uwiano na kushirikiana nasi kama viongozi ili tuilinde amani ambayo tayari ni nyeti sana hapa Kivu Kaskazini’.