Waziri Mkuu mpya Mamadou Oury Bah amekuwa mtu mashuhuri katika siasa za Guinea tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini.
Mamady Doumbouya alimpindua Rais Alpha Conde mnamo Septemba 2021.
Mamlaka ya mpito nchini Guinea inayoongozwa na junta imemteua aliyekuwa kiongozi wa upinzani na mwanauchumi Mamadou Oury Bah kuwa waziri mkuu, kwa mujibu wa amri iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumanne.
Mkongwe huyo wa kisiasa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuunda serikali huku kukiwa na mgomo mkuu usiojulikana uliozinduliwa wiki hii kutokana na matatizo makubwa ya kiuchumi na sera zinazodaiwa kuwa kandamizi za mamlaka za kijeshi.
Picha za televisheni zilionyesha Bah akila kiapo mbele ya Rais wa mpito Mamady Doumbouya, kamanda wa kikosi maalum ambaye alimuondoa madarakani aliyekuwa Rais Alpha Conde katika mapinduzi ya mwaka 2021.