Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb) amethibitisha kwamba Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), imeingia makubaliano na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa lengo la kupeleka huduma ya mawasiliano katika Kata ya Litapunga.
Mhe. Mha. Mahundi ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mhe. Anna Richard Lupembe (Mb) leo tarehe 08 Aprili, 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Mhe. Mha.Mahundi ameeleza kuwa katika jitihada hizo, Serikali kupitia TTCL inajenga mnara katika kijiji cha Kambuzi ‘A’ ambao utahudumia vijiji vya Kambuzi ‘A’ na Kambuzi ‘B’.
Mhe. Mha. Mahundi amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 kuanzia tarehe 13 Mei 2023, ambayo ilikuwa tarehe ya kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa mnara huo.