Wakati Tanzania ikitajwa kuwa mdau muhimu wa masoko ya kikanda ikiwemo afrika mashariki katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara dr Ashil Abdalah ametaka kufanyika utafiti juu ya matumizi ya mfumo wa teknolojia akili mnemba ilikuhakikisha mlaji anapatiwa huduma bora inayokidhi viwango.
Hayo yamesemwa na Katibu mkuu Dr Ashil Abdalah katika kilele cha maadhimisho ya siku haki ya mlaji duniani ambapo ameeleza matumizi ya mfumo wa akili mnemba katika utoaji wa huduma kwa mlaji kubainisha faida na athari zinazoweza kumlenga moja kwa moja mlaji ili kuwezesha watunga sera na sheria kuangalia namna bora ya kuja na suluhisho la kukabiliana na changamoto hizo.
Katibu Mkuu pia amesema kuwa Tanzania ni sehemu ya mdau muhimu katika masoko ya kikanda ya africa mashariki (SADC) soko huru la Afrika na masoko ya kimataifa ni muhimu kwa washiriki kujadiliana kwa kina ili kupata ufumbuzi wa pamoja juu ya changamoto zinazoweza kujitokeza katika ukuaji wa mabadiliko wa sayansi na teknolojia katika usambazaji wa bidhaa kwa mlaji.
Kwa upande wake mwanasheria mkuu wa serikali jaji Eliezer Felesh, amesema kwa mujibu wa sheria ya haki ya mlaji inapaswa kulindwa na kuwekewa mazingira mazuri ya ushindani kuanzia kwenye sekta ya uzalishaji viwandani.