Mgombea Mwenza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepanga kununua meli tano kubwa za uvuvi zitakazotumika kuvua samaki katika ukanda wa Pwani.
Mama Samia ambaye pia ni Makamu wa Rais, amesema ununuzi wa meli hizo unalenga kutoa fursa zaidi ya ajira hususani vijana na kuwawezesha Watanzania wanufaike na rasilimali za Taifa.
Amesema ununuzi wa meli hizo utakwenda pamoja na ujenzi wa bandari ya uvuvi ambazo meli zote zitakazovua kwenye eneo la bahari ya Tanzania zitatakiwa kutia nanga ili mapato stahiki ya serikali yapatikane.
Akizungumza na wananchi wa Nangurukuru, wakati akiwa njiani kuelekea Mtwara, amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa wizi uliokuwa ukifanywa na meli za uvuvi zinazovua samaki ukanda wa bahari ya Tanzania.
Kuhusu shida ya kivuko kutoka Mchinga moja hadi Mchinga mbili, Mama Samia amesema atatuma wataalamu wa vivuko kuangalia eneo hilo ili changamoto hiyo iweze kutatuliwa.
JAMAA ANG’ATWA NA NYOKA CHOONI AKITAZAMA VIDEO KWENYE SIMU “NILISIKIA UCHUNGU”