Ikiwa ni siku tano zimepita tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuhukumu aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake, Serikali imewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu hiyo.
Hukumu ya Malinzi na wenzake akiwemo Katibu wake, Celestine Mwesigwa
ilitolewa Desemba 11, 2019, ambapo Malinzi alitakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kwenda jela mwaka mmoja, huku Mwesigwa, akitakiwa kulipa faini ya Sh.M1milioni au kwenda jela miaka miwili.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wankyo Simon imebainisha kuwa leo, Desemba 16, 2019, kuwa upande wa mashtaka umewasilisha nia hiyo ya kukata rufaa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Maombi hayo ya rufaa yaiwasilishwa mahakamani hapo, Desemba 13, 2019.
Wakili Simon amedai kuwa wamewasilisha nia hiyo baada ya kutoridhishwa na hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde aliyekuwa akisikiliza shauri hilo katika makosa waliyotiwa hatiani washtakiwa hao.
Mbali na kuwasilisha nia ya kukata rufaa, pia wameomba wapatiwe nakala ya hukumu pamoja na mwenendo mzima wa kesi hiyo.
Kutoka na hukumu hiyo, Malinzi alitakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kwenda jela mwaka mmoja na Mwesigwa kulipa faini ya Sh 1milioni moja au jela miaka miwili, hata hivyo, washtakiwa hao walifanikiwa kulipa na kuachiwa huru Desemba 12.
wakati Malinzi na Mwesigwa wakitiwa hatiani, mahakama hiyo iliwaachia huru Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani wa shirikisho hilo, Flora Rauya, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka ju yao.
MKE APEWA MIMBA, MUMEWE KAZAWADIWA GARI LA MAMILIONI ASAMEHE