Serikali imetangaza kuanza kwa Combination mpya tano kwa ajili ya wanafunzi watakaoingia kidato cha tano mwaka 2021.
Lengo la kuongeza tahasusi hizo ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Combination hizo ni Fizikia, Hesabu na kompyuta (PMC); Kiswahili, French ,Chinese (KFC); Kiswahili, English, Chinese (KEC); Physical Education, Biology, Fine Art (PBF) na Physical Education, Geography, Economics (PGE).
“JAFO KAMA UMESHINDWA TUAMBIE, TAMISEMI MNACHUKUA FEDHA HAZIRUDI”- RAIS SAMIA AWASHA MOTO