Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamis Kigwangalla leo February 19, 2018 amefika katika msiba wa Mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Maftah ambaye alifariki baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye daladala na polisi waliokuwa wakitawanya wafuasi wa CHADEMA.
Waziri Kigwangalla amewataka wananchi kuacha kujiuliza nani amehusika katika tukio la kumpiga risasi bali kwasasa wajadili kuhusu msiba uliopo kwanza.
“Ndoto za binti huyu zimezimika ghafla, nimesikitika sana, nimekuja kujumuika na Watanzania wenzangu kumlilia Akwilina, nmeguswa na msiba tuendelee kumlilia sidhani kama ni wakati muafaka kuanza kunyoosheana vidole nani kafanya nini, hili halina umuhimu kwa sasa,” -Waziri Kigwangalla
UTEUZI ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO FEBRUARY 19,