Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amefanya ziara katika maeneo ambayo ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ‘Standar Gauge’ kutoka DSM mpaka Morogoro unaendelea na kusema ujenzi huo utagharimu Tilioni 2.6 na unategemewa kukamilika June, 2020.
“Ujenzi wa reli ya kisasa toka DSM mpaka Morogoro yenye urefu wa KM 300, mradi huu unajegwa kwa Tsh. Tilioni 2.6 na unagharamiwa na Serikali kwa asilimia mia moja, mpaka sasa wamefikia asilimia 5.86 ya ujenzi na imechelewa sababu ya mvua,”-Prof. Mbarawa
Tumepanga June 2020, reli hii Watanzania waweze kuitumia, katika ujenzi huu wafanyakazi 1750 wamepata kazi, kazi inaendelea vizuri na sisi tupo hapa kusimamia,” -Prof. Mbarawa
Lukuvi baada ya kufika Ilemela na kuamua kukagua mafaili mwenyewe (video)