Leo February 23, 2018 Upande wa Mashtaka umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ahirisho la mara mbili (siku 28) katika kesi inayowakabili vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili maarufu Dk.Ringo Tenga ili kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
Mbali na Dk. Tenga, washtakiwa wengine ni Mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Nyantori amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, ila wanaomba ahirisho la mara mbili sawa na siku 28 ili kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa aliusisitiza upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi kwa haraka ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi March 9, 2018.
Katika hati ya mashtaka kwa pamoja washtakiwa wanadaiwa walitenda kosa la kutakatisha fedha Dola za Marekani 3,282,741.12, huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa la udanganyifu.
Baada ya kifo cha AKWILINA Sheria inasemaje kwa vifo kama hivyo
Tido Mhando alivyowasili Mahakamani leo