Leo February 17 2018 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kuwa mtu mmoja amepigwa risasi wakati wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wanaandama February 16, 2018.
Wafuasi hao walikuwa wanaandamana kuelekea Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni kudai viapo vya Mawakala wa Chama hicho.
Eneo la Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na Polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia. Mambosasa amesema walizuia mabasi ya mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata mtu.
POLISI WALIVYODHIBITI WAANDAMANAJI WA WALIOKUWA WANAENDA KWA MKRUGENZI WA UCHAGUZI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA