Kutoka nchini Australia, leo March 23, 2018 inaelezwa kuwa Nyangumi takribani 150 wamekwama katika ufukwe wa bahari Magharibi mwa Australia na kusababisha kufungwa kwa muda kwa eneo hilo la ufukwe.
Idara ya Uvuvi nchini humo wameeleza kuwa wanahisi nyangumi hao wamekufa na hivyo imebidi wafunge ufukwe huo kwa muda kwa kuhofia papa wanaweza kuleta madhara kwenye eneo hilo.
Idara hiyo imeeleza kuwa papa huvutiwa na viumbe waliokufa hivyo nyangumi hao ambao inaaminika wamekufa wanaweza kufanya papa wasogee eneo hilo la ufukwe na kusababisha madhara makubwa zaidi.
Jinsi Mtanzania alivyoanza kubadilisha Makaratasi (Taka ngumu) kuwa Magodoro