Tunayo stori kutokea kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambapo amesema ni kawaida yake kutoa maelekezo baada ya kutembelea na kufanya ukaguzi katika vituo vya Polisi hasa Askari wanapotuhumiwa kuwabambikizia kesi mahabusu.
Waziri Lugola amesema kuwa moja kati ya vituo alivyovitembelea ni Sitakishari ambapo amebaini kasoro na ametoa maelekezo baada ya kuwahoji mahabusu kutokana na tuhuma za Polisi kuwabambikia kesi.
“Kituo hiki ni moja kati ya vile ambavyo wananchi wanalalamikia kwamba vinabambikia watu kesi, hivyo leo nimekuja nimeingia mahabusu na kuwahoji kuhusu muda waliokaa na zipo kasoro na nimetoa maagizo,“amesema.