Ni July 15, 2016 ambapo Malkia wa uswazi, Sara Kaisi aka Shaa amefunguka kupitia Ayo TV na kuelezea sababu za kuondoka kwenye uongozi wake wa zamani.
Akizungumza na Ayo TV staa huyo alisema…’Nimekuwa na ndoto ya muda mrefu kama ya miaka mitano iliyopita tumeona wasanii ambao niliokuwa nao MJ Records wakina Izzo Bizness amesimama mwenyewe ukija kwa Quick Rocka nae kafungua studio kwahiyo huu ni muda wangu’– Shaa
‘Maamuzi ya mimi kwenda kwenye uongozi wakina Tale ilikuwa baada ya mimi mkataba wangu kumalizika kwenye lebo ya Unity Entertainment ya AY nilifanya nao kazi nzuri mpaka zingine zikakubalika ila maamuzi yangu kwa 2016 kazi zangu zitasimamiwa chini ya record label yangu’- Shaa
ULIIKOSA HII YA BARAKA DA PRINCE KUHUSU UJAUZITO WA NAJ BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA