Moja ya mijadala mikubwa iliyozuka katika Bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ni pamoja na taarifa ya kufutwa kodi ya magari yaani ‘Road License’…na kisha Serikali kusema itaongeza kiasi cha shilingi 40 kwa kila lita ya mafuta jambo ambalo baadhi ya Wabunge walipinga na kusema itasababisha gharama za mafuta kuwa kubwa zaidi.
Lakini hii ilikuwa tofauti kwa Mbunge wa Gairo Ahmed Shabiby ambaye tangu mwanzo alieleza kuwa wasitegemee gharama kuongezeka licha ya baadhi kumpinga
Na sasa Good News hii kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA ambao wametangaza kushuka kwa bei mpya za mafuta ya vyombo vya moyo ikiwemo magari na mashine. Bei hizi elekezi zinaanza kutumika rasmi July 1, 2017.
Millardayo.com inaye Mbunge Ahmed Shabiby kwenye exclusive interview akiongea ya moyoni baada ya EWURA kushusha bei ya mafuta unaweza kumsikiliza kwenye hii sauti hapa chini….
VIDEO: Makubwa aliyochangia Shabiby ndani ya dk 10 kwenye Bajeti Kuu 2017/18