Shabiki wa kandanda aliyemtusi mchezaji na kufanya kitendo cha kibaguzi wakati wa mchezo katika ligi ya daraja la tatu nchini Uingereza alihukumiwa kifungo cha miezi tisa jela siku ya Alhamisi.
Ryan Ferguson, 24, wa Liverpool, alikiri kosa la unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi kwa kumtusi mchezaji wa Forest Green Jordon Garrick, ambaye ni Mweusi.
Tukio hilo lilitokea Aprili mwaka jana kwenye mchezo wa nyumbani wa Forest dhidi ya Fleetwood.
“Vitendo vya Ferguson vilikuwa vibaya na ni jambo ambalo hakuna hata mmoja wetu anayepaswa kushuhudia kwenye mechi ya soka – iwe mashabiki, wafanyakazi, polisi au wachezaji wenyewe,” alisema Douglas Mackay, mwendesha mashtaka mkuu wa kitaifa wa Huduma ya Mashtaka ya Kitaifa.
“Adhabu ambayo imetolewa na inapaswa kuwa mwamko kwa mashabiki wowote ambao wanadhani inaweza kukubalika kuvunja sheria wakati wa mechi.”