Shabiki wa Tottenham amepigwa marufuku ya miaka mitatu kutohudhuria mechi za soka baada ya kukejeli maafa ya Hillsborough mwezi Aprili.
Ishara hiyo mbaya ilifanyika wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Spurs dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield mnamo Aprili 30, ambayo wenyeji walishinda.
Siku ya Jumanne, kitengo cha huduma ya mashtaka iligundua kuwa Kieron Darlow, 25, alikuwa ametoa ishara kwa wafuasi wa Liverpool yaani ishara za kukejeli mkasa huo.
Tukio hilo baya lilishuhudia mashabiki 97 wa mpira wa miguu wakipoteza maisha katika msongamano wa watu kwenye Uwanja wa Sheffield Wednesday’s Hillsborough mnamo 1989 huku baraza la uchunguzi mnamo 2016 liliamua kwamba vifo hivyo havikuwa halali baada ya orodha ya makosa ya polisi wakati huo.
Andrew Page, wa CPS Mersey Cheshire, alisema katika taarifa yake: “Darlow alikiri kuwaonyesha ishara mashabiki wa Liverpool na kwamba hii ilikuwa kumbukumbu ya maafa ya Hillsborough na alikiri kwamba hii ilikuwa ni kuashiria kwamba mashabiki bila tiketi walikuwa wamesukumana kuingia kwenye mechi na kusababisha maafa na amekuwa na lawama kwa kuponda namna ambayo ilisababisha vifo vingi.
“Alikubali mahakamani kwamba ilikuwa nia yake kwamba mashabiki wa Liverpool wanapaswa kuona hili na kwamba litawasababishia manyanyaso, hofu na mafadhaiko. Darlow alijua anachofanya na ilifanyika akijua athari ya msiba wa Hillsborough ilikuwa ni mashabiki wa Liverpool na jiji la Liverpool lakini alifanya hivyo makusudi.
“Tabia ya aina hii siyo tu kwamba haikubaliki kimaadili, bali ni ya jinai.
Tunatumai shitaka hili linatoa ujumbe kwa mashabiki wote wa soka kuwa tabia zao kwenye michezo ya soka ni muhimu na iwapo itaingia katika uhalifu, watakutana na nguvu kamili ya sheria.”
Sio mara ya kwanza kwa maafa ya Hillsborough kutumiwa katika ujumbe wa kuchukiza kutoka kwa mashabiki wa wapinzani.
Kabla ya fainali ya Kombe la FA mapema mwezi huu ambapo Liverpool hata hawakucheza shabiki mmoja wa Manchester United alirejelea wahasiriwa 97 lililoonekan nyuma ya shati yake pamoja na maneno “haitoshi”.