Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries imemkabidhi zawadi ya gari aina ya Toyota IST Mshindi Shamimu Mushi ambaye ameibuka Mshindi kwenye promosheni ya kapu la Wana iliyokua ikiendeshwa na Kampuni hiyo kupitia bia yake ya Plisner Lager.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hiyo iliyofanyika jijini Arusha, Meneja Masoko wa SBL kanda ya Kaskazini Andrew Msiagi alisema “tumefika Arusha kwa ajili ya kufanya makabidhiano ya zawadi hii kubwa, ninafuraha zaidi kwa Mwanamke kuibuka Mshindi wa mwisho wa kampeni yetu na hii inaonyesha kuwa chapa yetu ya Pilsner inapendwa na Watu wa kila aina.”
Promosheni hii ilianzishwa ili kuwazawadia Watumiaji wa Pilsner wanaofanya kazi kwa bidii katika Kanda za Ziwa, Kusini na Kaskazini ili kuwasaidia kubadili maisha yao kwa namna moja au nyingine kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali kuanzia simu janja, TV, pikipiki hadi gari ambalo ndio zawadi kuu ambapo kwa ujumla SBL iliwekeza TZS. milioni 36 kwa ajili ya kuwazawadia Wachapakazi wanaofanya kazi kwa bidii.
Kampuni ya SBL ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries na sasa SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania na chapa zake za bia zikichukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo huku ikiwa na mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza, na Moshi.