Mfanyabiashara muuza Matunda anayedaiwa kunajisi wanafunzi katika Shule za Chekechea na Msingi Minazi Mirefu na Airwing atasomewa hoja za awali Agosti 18, 2022 baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika na yeye kuachiwa kwa dhamana.
Juni 12 mahakama ya Wilaya ya Ilala ilimpandisha kizimbani Joshua Simangwe (66) Mkazi wa Kipunguni Ukonga kwa shtaka la kumlawiti mtoto wa miaka nane(jina limehifadhiwa).
Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu Nestory Baro, Mwendesha Mashtaka wa Serikali Joyce Nyumayo alisema katika kesi ya Msingi inadaiwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe isiyojulikana Mei, 2022 katika eneo la Banana Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam.