Beki wa klabu ya Manchester United mwenye umri wa miaka 20 Luke Shaw ambaye alivunjika mguu katika mechi ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, tayari amepata matibabu na kuthibitisha kurejea Manchester.
Luke Shaw ambaye alivunjika mguu dakika ya 15 ya mchezo baada ya kufanyiwa tackling na beki wa klabu ya PSV Eindhoven Hector Moreno, tukio lililopelekea kuvunjika mguu wake wa kulia na kupelekwa katika hospitali ya St Anna iliyopo Eindhoven Uholanzi, tayari amefanyiwa upasuaji na hali yake inaendelea vizuri.
Kupitia post aliyoweka katika account yake ya instagram Luke Shaw amewashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali ya St Anna na kuthibitisha kuwa tayari kurejea Manchester licha ya kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita akiuguza jeraha lake la mguu. Luke Shaw amewasili Manchester mchana wa September 19 akitokea Eindhoven.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos