Binti mmoja nchini Canada ajulikanaye kama Charlie Lagarde ameshinda bahati nasibu kubwa kwenye siku ya birthday yake na kufanya watu waseme bahati nasibu hiyo imebadilisha maisha yake yote.
Charlie kwenye kusheherekea birthday yake ya miaka 18 mnamo March 14, 2018 alinunua tiketi ya bahati nasibu ikiwa ndio mara yake ya kwanza, pamoja na chupa ya mvinyo.
Binti huyu ametangazwa kushinda na alitakiwa kuchagua kuchukua kitita cha Dola za Marekani 780,000 ambayo ni sawa na Shilingi bilioni 1.8 kwa mkupuo au kupewa Dola 1000 sawa na Shilingi milioni 2.4 kila wiki kwa maisha yake yote.
Charlie alichagua kulipwa pesa hiyo kwa kila wiki kwa maisha yake yote yaliyobaki duniani.
“Wananchi wanashangilia bila kujua lile ni bomu” – Mwenyekiti CCM Mtwara