Kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ufauli kwa Wnaafunzi wa Kidato cha nne mwaka 2022, Uongozi wa Shule ya Kiislamu ya Alhkima umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Al Hikma Foundation, Sheikh Nurdin Kishki amesema katika Matokeo ya kidato cha nne shule ya Alhkima ya wanaume iliweza kushika nafasi ya pili katika shule za Kiislamu Tanzania kwa matokea ya kidato cha nne ya mwaka 2022.
Kupitia hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri, Sheikh Kishk amesema;
“Katika shule zote hakuna mwanafunzi aliyepata divisioni zero wala four, na kwa upande wa alhkima ya wanawake wanafunzi 26 walipata division 1, wanafunzi 44 walipata divison 2 na wanafunzi 1 alipata divisioni 3 na kwa shule ya alhkima ya wanaume wanafunzi 61 walipata division 1 na wanafunzi 18 walipata division 2,” amesema shekh Kishki
Naye Afisa Elimu wa Sekondari wilaya ya Temeke, Abdul Buheti ametoa rai kwa wanafunzi hao waliofaulu kuhakikisha wanaenda kwenye shule za sekondari za serikali kwa kidato cha tano watakazo pangiwa ili wawe chachu ya kuwafunza wanafunzi wengine maadili mazuri waliopata shuleni hapo hasa kwa upande wa dini.
“Rais Samia ametoa zaidi ya Bilioni 4 kwaajili ya ujenzi wa Madarasa 207 ya shule za sekondari Wilaya ya Temeke,”amesema Buheti.