Kutoka Arusha taarifa ambayo imetangazwa kupitia Leo tena ambayo imetolewa kama breaking news ni kuhusu Sheikh wa msikiti wa Qiblatan Sudi Ally Sudi (37) uliopo eneo la Kilombero jijini Arusha kulipuliwa na bomu la kurushwa kwa mkono nyumbani kwake wakati akila daku.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sheikh Sudi amejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili na sehemu za mapajani pamoja na Kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Akiwa kwenye hospitali ya mkoa Mount Meru, Sudi amesema ‘nilijikuta tu nimeumia baada ya kutupwa bomu nyumbani kwangu na kuumia kwenye miguu’
Muhaji Kifea (38) mkaazi wa Dar es salaam ambae alikua na Sheikh wakati huo amesema ‘jana nilikua nimetokea Nairobi hivyo akawa amenitengea chakula nikawa napata daku pale na wakati huohuo ndio bomu likanilipukia na ilikua kama saa tano usiku hivi, walilirusha kupitia dirishani na tayari walikua na vitisho juu yake, hata kwenye kutupa bomu walitaka kumdhuru yeye sio mimi’
Hii taarifa imekuja wakati Mufti Issa Bin Shaaban Simba akiwa ametoa tamko juu ya mgogoro wa muda mrefu wa uongozi kwenye msikiti mkuu wa Ijumaa wa mkoa wa Arusha na msikiti mdogo na kuweka wazi viongozi wanaostahili kuiongoza misikiti hiyo kisheria.
Tamko amelitoa mbele ya baadhi ya Waumini na Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha Sheikh na kusema viongozi wapya waliopewa jukumu la kuongoza misikiti hiyo ambao waliondolewa na kikundi cha Waumini, wako kwa mujibu wa sheria na ndio wanaotambulika na sio vinginevyo.
Hata hivyo baada ya Sheikh Mkuu kutoa tamko hilo viongozi walioondolewa madarakani wamesema hawatambui tamko la sheikh mkuu Mufti Issa Shaaban kwani limetolewa wakati tayari kesi iko Mahakamani.
Sheik Simba alisema msikiti mkuu wa Ijumaa utaongozwa na Sheikh wa mkoa Shaban Bin Jumaa Abdallah na kaimu katibu wa mkoa Ustadh Abdallah Masoud na mwenyekiti wa halmashauri Ustadh Mohamed Juma Marawi na msikiti wa Masjid Quba utaongozwa na Sheikh Hassan Waziri ambae ni imamu na Abubakar Sharif huku mweka hazina akiwa ni Chohan Jumbe.
Niko tayari kukutumia wakati wowote kila kinachonifikia kwenye page zako za twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB