Serikali kupitia wizara ya Uchukuzi imeanza mchakato wa mabadiliko ya sheria inayosimamia mamlaka ya Usimamizi wa usafiri Ardhini LATRA juu ya adhabu za Mamlaka hiyo inayoanzia laki mbili na nusu kwa vyombo vyote vya usafiri bila kujali ukubwa wa chombo au kosa na badala yake iweze kusimamia zaidi kueleimisha na kutoa leseni na endapo muhusika akiendelea na ukosaji basi adhabu itokane na daraja alilopo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo na Kaimu Mkurugenzi wa usafiri barabarani wa wizara ya uchukuzi Andrew Magombana ambao wamesema sheria inayosimamia Mamlaka ya LATRA wadau wengi wameipigia kelele kua inawatesakwa kutoa adhabu badala ya kutoa elimu zaidi elimu hivyo kuomba adhabu zipunguzwe lakini kutoingiliana na taasisi zingine kama jeshi la Polisi ambao nao wanasimamia sheria hizo hizo.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Habibu Suluo amesema sheria ya sasa unakuta watumishi wengi wa taasisi hiyo wanasimamia kukusanya mapato ambayo yapo kisheria kuliko kutoa elimu na upatikanaji leseni hivyo mabadaliko ya sheria hayo yatasaidia kutatua vilio ya watoa huduma ya usafiri kwani kwasasa mtu anayemiliki guta Faini yake inafanana na mtu ana miliki lori au basi au daladala hivyo wameona wasikilize vilio hivyo ili ufanisi wa kazi Kwa pande zote uwe sawa kusiwe na malalamiko.
“Adhabu zinawaumiza wawekezaji hawa wa sekta binafsi,utakuta karibu asilimia 30 ya mapato ya latra yanatokana na adhabu sasa hili si jambo jema, mafano mdogo Roli lile linabeba tani 56 linapofanya kosa adhabu yake inafika 250000 lakini unakupa Toyo inayobeba mzigo ambayo imepewa leseni nayo ikifanya kosa adhabu yake hiyohiyo kwasababu kanuni imesema”
“hata ukienda kwenye mabasi ya mjini (daladala) na yale ya mkoa adhabu ni sawa huu uwekezaji unatofautiana unamuumizakwa adhabu hizi ndio mana tukasema tuangalie uwekezaji na adhabu ile isije kumuumiza akafunga na biashara”
Aidha serikali imetoa siku saba kwa wadau wa usafirishaji kutoa maoni yao kabla ya mabadiliko hayo ya kanuni hayaja anza kufanyiwa kazi baada ya mwaka mpya wa kifedha wa Serikali