Madagascar ilitangaza sheria ya kutotoka nje siku ya Jumatano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo, inayotumika usiku mmoja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais, ambao utafanyika baada ya wito wa kuususia kutoka kwa viongozi wakuu wa upinzani.
Wapiga kura milioni 11 waliojiandikisha wanaitwa kupiga kura siku ya Alhamisi kumchagua rais wao mpya. Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 6 asubuhi saa za Madagascar. Baada ya mwezi mmoja na nusu wa maandamano katika mitaa ya Antananarivo kwa wito wa upinzani, gavana wa mji mkuu, Jenerali Angelo Ravelonarivo, ameshutumu “vitendo vya hujuma” siku ya Jumatano.
“Kutokana na vitendo mbalimbali vya hujuma vilivyotokea” Jumanne jioni, “nitatoa uamuzi hivi karibuni wa kutaganzwa sheria ya kutotoka nje kutoka saa 9:00 usiku hadi saa 4:00 usiku (Alfajiri),” ametangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuchapishwa kwa nakala hiyo. Akirejelea “kuchomwa kwa kituo cha kupigia kura” na “kuharibiwa kwa vifaa mbalimbali vya uchaguzi”, gavana huyo ameonya dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha watu kukamatwa “katika kipindi hiki cha uchaguzi”.
Wagombea 13 wanawania kiti cha urais, akiwemo rais anayemaliza muda wake Andry Rajoelina, mwenye umri wa miaka 49. Wagombea kumi wa upinzani walikusanyika kwa pamoja, wakiwemo marais wa zamani Hery Rajaonarimampianina na Marc Ravalomanana, waliwataka wapiga kura siku ya Jumanne kutopiga kura.