Kwenye zile stori za Hekaheka leo inatokea maeneo ya Kawe, Dar es salaam.
Kuna jirani mmoja ambaye ni mwanamke aliamua kuziba njia ili watu wasipite karibu na nyumba yake..kilichowachosha majirani zake kila akiulizwa alikuwa anapiga watu kwa kutumia nondo na kisu.
Ilifika mahali wananchi walichoshwa na tabia yake hasa wanawake wenzake na kuamua kuandamana hadi kituo cha redio Clouds kuomba msaada baada ya Polisi kudaiwa kushindwa kuwatatulia kero yao.
Mama mmoja ambaye ni shuhuda anasimulia na kusema mama huyo amekuwa haelewani na mtu yoyote mtaani kwao na anapiga majirani zake pamoja na watoto.
Amekuwa na tabia ya kuwasubiri majirani zake na kuanza kuwapiga kwa silaha kama mawe na kisu..
Kwa sasa amepelekwa Polisi, Kawe lakini kila akipelekwa Polisi anatolewa na kuwaringishia majirani zake kuwa polisi hawawezi kumfanya lolote na kuendelea na tabia hiyo.
Samahani sauti ya majirani wakizungumza na Geah Habib jinsi mwanamke huyo anavyowanyima raha mtaani kwao imeshindikana kusikika hapa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE