Chuo chamipango kupitia ufadhiri wa Mradi wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa ( UNDP ) Tanzania, inafanya tafiti ya kuanisha vyanzo vya mapato ya halmashauri tisa , saba Tanzania bara na mbili visiwani Zanzibar .
Tafiti zitaambatana na elimu ya uandikaji maandiko ya kupata pesa ya kuanzisha makampuni kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri na mtu binafsi.
Akizungumza wakati wa Kikao kazi mjini Morogoro mhadhiri Mwandamizi Chuo kikuu Mipango ya Maendeleo vijijini kituo Cha Mafunzo Kanda ya Ziwa Daktari Bonamax Mbasa amesema halmashuri nyingi zinakabiliwa na changamoto ya uelewa wa maandiko ya fedha za miradi.
Mbassa anasema kutokana kuwepo kwa changamoto hiyo chuo hicho kinawajibu wa kubini mbinu na kutoa elimu kwa halmashauri ili kuhakikisha wanakua na miradi inayoingiza pesa .
Anasema Kila Mtanzania anatakiwa awe na maisha Bora hivyo mradi huo wa kutoa elimu kwa halmashauri kuongeza miradi utasaidia kwani ajira zitaongezeka na jamii itapata fedha .
” Halmashauri hizo zitakazo fikiwa na mradi huo ni pamoja na songea,Ruangwa,Mlele,Nzega,MtwaraMikindani,Mlimba,Micheweni,Magharibi A na Njombe ” amesema Bonamax.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji Manipsaa Songea Dokta Fedrick Damas anasema mradi huo utasaidia kwani halmashauri nyingi zinamiradi ambayo inaandaliwa isiyoingiza faida hivyo itasaidia.
Anasema ni lazima miradi inayoanzishwa inakua inaendelezwa pamoja na kukarabatiwa ili iwe na faida hasa katika ukusanyaji mapato.