Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yao huku wakiwa na mtazamo chanya katika shughuli zao ili kufikia mafanikio kiuchumi.
RC Mwanri ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vijana linalohusisha vijana wa Mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida na Kigoma litakalodumu kwa siku mbili likiwa na lengo la kuwavutia vijana kujishughulisha katika kilimo.