Msemaji wa Familia ya Marehemu Akwilina Akwilini, Festo Kawishe ametoa ufafanuzi kuhusu kitu kilichosababisha wao kugoma kuupokea mwili katika hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya February 19, 2018.
Akiongea na AyoTV na millardayo.com Kawishe amesema walitaka kwanza kujiridhisha ni kipi hasa kimemuua ndugu yao Akwilina Akwilini kabla ya kuendelea na mazishi.
“Tulichowaambia Polisi ni kwamba msimamo wetu tunataka kujua kipi kimemuua ndugu yetu, tukataka uchunguzi ufanyike, Doctor ameniambia alipata jeraha la kitu chenye ncha kali kama goroli, mimi nikahisi ni Bunduki na nikamwambia kama ndicho utaandika Doctor mimi nitaenda kumzika ndugu yetu” -Festo Kawishe
MSIBA WA AKWILINA: Msemaji wa Familia kazungumza kuhusu Serikali kugharamia Mazishi