Katika kuadhimisha miaka 50 ya huduma nchini Tanzania na waanzilishi wake, Shirika la AHEAD limeandaa kongamano la siku mbili lililopewa jina la “Ubora wa Huduma za Afya 2024” linalowaleta pamoja wadau mbalimbali wa afya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hili kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Julius Nyerere, Mkurugenzi wa Shirika la AHEAD, Dk Donna Williams-Ngirwa alisema imekuwa safari ya kustaajabisha kwao kama familia wanavyosimlia jinsi walivyohamia Tanzania kutoka nchini Marekani Julai 1974 na baadaye wazazi wao, Dk na Bi Irving Williams walianzisha Shirika la Ujasiri katika Afya, Elimu, na Maendeleo ya Kilimo, shirika lisilola la kiserikali na lisilotengeneza faida linalolenga nguzo tatu za maendeleo, yaani afya, elimu na kilimo.
“Sisi kama watoto wa waanzilishi wa Shirika la AHEAD tunaendelea na kazi ambayo wazazi wetu waliianzisha kuhakikisha kwamba programu za kudumisha maisha zinafika hadi maeneo ya mbali zaidi na yenye uhaba wa rasilimali na zinakuwa endelevu.
Katika kuadhimisha miaka 50 ya mafanikio ya kihistoria, tunaona fahari leo kuwa mwenyeji wa kongamano hili la Ubora wa Afya lenye dhamira, “Kuendeleza afya kwa njia ya uongozi, diplomasia, uvumbuzi na ushirikiano,” alisema.
Kulingana na Dk Williams-Ngirwa, malengo ya kongamano hili, pamoja na mambo mengine, kujadili na kubadilishana maarifa juu ya mikakati yenye matokeo yanayotarajiwa ya uongozi katika afya na afya ya diplomasia, kwa kusisitiza nafasi ya viongozi katika kuleta mabadiliko chanya na kukuza afya ya usawa.
Kongamano hili pia, kulingana na Mkurugenzi, linaangalia teknolojia za kisasa, maendeleo ya matibabu na utendaji wa kibunifu ambao unabadilisha mustakabali wa utoaji wa huduma za afya na unakuza ubia na ushirikiano miongoni mwa watoa huduma za afya na mashirika, taasisi za kiserikali na wadau wa kimataifa kushughulikia changamoto za afya duniani.
“Kongamano linalenga kuwa chachu ya mabadiliko katika sekta ya afya nchini Tanzania, likisisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora za afya kwa watu wetu na kwa kutumia watu wetu,” alisema Mkurugenzi.
“Tanzania ina watoa huduma bora wa afya. Tunahakikishaje wananchi wote wanapata huduma bora?”
Kongamano lilipata kibali kutoka Wizara ya Afya na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, pande zote hizi mbili zikipongeza nafasi ya Shirika la AHEAD katika kukuza maendeleo ndani ya sekta ya afya na kwa kuandaa kongamano hili.
Mada zilizojadiliwa na wazungumzaji mbalimbali katika kongamano ni pamoja na afya ya akili, mfumo wa afya ya kinywa, matibabu ya watoto (na magonjwa yao) na radiolojia, huku hotuba muhimu ikitolewa na Dk Winnie Mpanju-Shumbusho, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani na mwanzilishi wa Shirika la AHEAD Tanzania.
Pamoja na kuwaleta mamia ya watu wanaojitolea kufanya kazi vijijini, Shirika la AHEAD limekuwa mfano wa kuigwa katika kukuza diplomasia ya watu, wakati huo huo likichangia kwa kiasi kikubwa jitihada za Tanzania katika kupunguza vifo vya uzazi, kuongeza viwango vya chanjo, na kusaidia katika miradi mingine mingi inayotekelezwa vijijini katika wilaya za Meatu, Kishapu, Kisarawe na miradi yao ya sasa huko Maruku, Bukoba