Shirika la NIC Insurance leo limetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwakwe kutoa huduma za bima kwa Watanzania.
Kama washirika wa NIC Insurance, Klabu ya Young Africans imeungana nao kusherehekea kilele cha miaka hii ya kumbukumbu.
Kwa niaba ya Uongozi wa Young Africans, Bwana Andre Mtine, Mkurugenzi Mtendaji wetu amekabidhi zawadi ya keki na jezi iliyosainiwa na Wachezaji wetu kwa NIC Insurance kama ishara ya kuenzi siku hii muhimu katika historia yao.
“Tumeingia mkataba wa udhamini na Young Africans SC hivyo kwenye mipango na mikakati yetu tutashirikiana nao kwa kiasi kikubwa, tunatambua kuwa hawa ndio washirika wetu wakubwa hivyo tutashiriki hata kwenye baadhi ya mikakati yao pia ili kuhakikisha tunasonga mbele” Elirehema Doriye Mkurugenzi Mtendaji NIC Insurance
“Nawashukuru sana ndugu zetu wa Young Africans SC kwa kuungana nasi kwenye siku hii ya kutimiza miaka 60 ya Taasisi yetu.
Ni matajarajio yetu tutaendelea kuwa bega kwa bega na nimepokea salamu za Rais wa Young Africans SC Eng Hersi Said, nimhakikishie tunajivunia sana uwepo wao kwetu.” Elirehema Doriye Mkurugenzi Mtendaji NIC Insurance.
‘Tunawashukuru sana NIC Insurance kwa kutushirikisha kwenye hafla yao ya kutimizia miaka 60, sisi kama klabu tunatambua kuwa NIC Insurance ni chapa namba moja, tunathamini sana mchango wao kwetu na kwa jamii wanayoihudumia’– Andre Mtine – CEO Young Africans SC
‘Ni heshima kubwa sana kufanya kazi na kampuni kubwa kama hii, Kwa upande wetu nasi tuna fahamu kuwa NIC wanajivunia kufanya kazi na sisi kwa pamoja tutapiga hatua kubwa.” Andre Mtine – CEO Young Africans SC