Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesitisha huduma za usafiri wa treni ya abiria na mizigo kutoka DSM kwenda Dodoma kutokana na uharibifu wa reli uliosababishwa na mafuriko maeneo ya Kilosa, Igandu, Dodoma na Makutupora.
“Kutokana na hali hiyo ya uharibifu Wahandisi wa TRC wako katika maeneo mbalimbali yaliyoharibika kufanya tathmini halisi ya gharama za miundombinu ya reli iliyoathirika, matengenezo ya muda mfupi yanaendelea”– Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa
Masanja amesema maeneo yaliyopata uharibifu mkubwa ni Kilosa, Gulwe(Mpwapwa), Igandu, Zuzu na Makutupora.
WALIOTAJWA NA MAGUFULI KUPEWA LAPTOP NA DOLA 800 MKATABA ULIOMG’OA LUGOLA WAITWA TAKUKURU