Baada ya miaka mitatu ya hali ya hewa ya baridi ya La Niña, WMO ilitangaza kuwa El Niño sasa inaendelea na ina uwezekano wa asilimia 90 wa kuendelea hadi mwisho wa mwaka kwa nguvu za wastani au zaidi.
Rekodi za halijoto tayari zinavunjwa na El Niño inaweza kusukuma ulimwengu kupita rekodi mpya ya wastani ya joto.
“El Niño kwa kawaida inahusishwa na viwango vya joto vinavyovunja rekodi katika kiwango cha kimataifa na ikiwa hii itatokea mwaka wa 2023 au 2024 bado haijajulikana, lakini kuna uwezekano mkubwa, nadhani,” anasema Carlo Buontempo, mkurugenzi wa Copernicus wa EU. Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi.
Akizungungumza kupitia mtandao akiwa jijini Geneva Uswisi Dkt. Maria Neira ambaye ni Mkurugenzi wa Mazingira, mabadiliko ya tabianci na afya wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa, utabiri wa hivi karibuni unaonesha kuwa hali ya El Niño sasa iko na inatarajiwa kufikia kilele chake kati ya mwezi Septemba 2023 na Februari 2024.
“El Niño inaweza kusababisha matukio mbalimbali ya hali mbaya ya hewa, ikiwa ni pamoja na ukame, mafuriko, vimbunga, na mawimbi ya joto, ambayo yote ni hatari kwa afya ya binadamu.” Amesema Dkt Neira.
El Niño inatarajiwa kuathiri maeneo mengi ulimwenguni lakini athari kubwa zaidi zitaonekana kwenye maeneo yenye hali ya ya joto, ikiwa ni pamoja na nchi na maeneo ya Afrika, Amerika ya Kusin, pamoja na Kusini na Kusini-Mashariki mwa Asia ambako huathirika zaidi na majanga ya kimaumbile.