Katika kuendelea kupinga ukatili ndani ya Mkoa wa Geita, Shirika la Plan International Mkoa wa Geita limetoa Baiskeli Mia 500 kwa wanafunzi wa shule za Sekondari ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu hali ambayo imekuwa ikiwapa changamoto na kupelekea kupata Ujauzito kutokana na ushawishi huku wengine wakiachana Masomo .
Akizungumza mara baada ya kukabidhi Baiskeli hizo Mkuu wa Wilaya ya Geita Willson Shimo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita shimo amelipongeza shirika hilo ambavyo wamekuwa wakiendelea kuunga mkono Jitihada katika kushirikiana na Serikali katika kuinua Mchango wa sekta ya elimu ndani ya Mkoa wa Geita.
“Katika utekelezaji wa mradi wa kuwezesha wasichana kuendelea na masomo yaani KAGIS Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Plan International wanakwenda kusaidia wasichana wapatao 2000 wa ndani ya shule kutoka Mkoa wa Geita na kigoma kupata Baiskeli kwa ajili ya usafiri, ” Mkuu wa Wilaya.
Shimo amesema Basikeli Baiskeli mia 300 zitasalia ndani ya Mkoa wa geita na Baisikeli Mia 200, zikipelekwa Mkoani Kigoma kwa ajili ya Matumizi ya wanafunzi wa Mkoa huo, Shimo amewataka wazazi pamoja na walezi kuzitumia Baiskeli hizo kwenda kuzitumia kwa Malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Peter Mwakabwale ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi ya Plan International nchini amesema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na washirika kutoka nchini Canada unalenga kutimiza malengo ya wizara ya Elimu na Teknolojia katika kumlinda msichana na kukabiliana na kukatishwa masomo yao.
“Sekta hii ya elimu imekumbwa na changamoto mbalimbali hususani hasa wa kike moja wapo ya changamoto hii ni kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni hasa kwa shule ya sekondari ambao wanasababisha wasichana hawa kukabiliana na hatari pamoja na vishawishi vingi vinavyopelekea wao kukatisha masomo yao mara nyingi wamekuwa wakikatishwa tamaa na wametawaliwa na hofu ya kuadhibiwa kuchelewa kufika baada ya kutembea mda mrefu, ” Mkurugenzi Plan International Nchini.
Nao Baadhi ya wanafunzi hao waliokabidhiwa Baiskeli hizo wamekili kukumbana na Vishawishi mbalimbali wanapokuwa wakitembea umbali mrefu kutoka Nyumbani kuelekea shuleni huku wakilipongeza shirika la Plan International kupitia Mradi wa KAGIS kwa kuona umuhimu wa kuwasadia wanafunzi hao kutoka Mikoa miwili ukiwemo Mkoa wa Geita na Kigoma.