Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) limewataka wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga mjini Iringa kukomesha migogoro inayowagawa ili wawe na sauti moja katika kushughulikia masuala yao.
Wito huu umetolewa leo, na Katibu Mkuu wa SHIUMA Taifa, Venatus Magayane katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Highlands Hall, Manispaa ya Iringa.
Katika kongamano hilo, Magaye alikiri kuwepo kwa tofauti kati yake na Naibu Katibu Mkuu wa SHIUMA Taifa, Joseph Mwanakijiji, ambaye pia alikuwa kiongozi wa Machinga Iringa. Alieleza kuwa baada ya majadiliano ya kina, wamekubaliana kumaliza tofauti zao na kufuta kesi zote zilizokuwa mahakamani kati yao.
Mwanakijiji pia alisisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa machinga wa Iringa, akisema kuwa ni muhimu kujitahidi pamoja ili kunufaika na fursa nyingi na mipango ya serikali inayowalenga.
“Machinga wa Iringa tunapaswa kuiga mfano wa mapatano haya na kuvunja makundi yote ili kujenga nguvu ya pamoja,” alisema Mwanakijiji.